Viwanda, Biashara na Masoko
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia 15 mwaka 2015 kwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta za viwanda, biashara na masoko kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia 15 mwaka 2015  kwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta za viwanda, biashara na masoko kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

  1. Kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji na biashara katika soko la ushindani.
  2. Kujenga na kuimarisha ujuzi katika biashara na kuweka msukumo zaidi katika kutumia fursa za masoko.
  3. Kujenga mifumo imara ya viwanda, biashara na masoko yenye kuendeleza na kukuza mauzo nje.
  4. Kuimarisha kifedha Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) ili kiwe chombo madhubuti cha kuchochea mapinduzi ya viwanda nchini kwa kutoa mikopo ya muda mrefu na riba nafuu kwa wawekezaji wakubwa, wa kati na wadogo nchini kote.
  5. Kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma, Chuma cha Liganga na viwanda vya kemikali na mbolea katika Kanda za Maendeleo kikiwemo kiwanda cha mbolea aina ya UREA mkoani Mtwara na kuwezesha kiwanda cha Minjingu kuzalisha mbolea bora ya NPK na MPR ili kufikia lengo lililowekwa.
  6. Kuimarisha uzalishaji mali viwandani kwa kuvifufua na kuviendeleza kwa teknolojia ya kisasa viwanda vyote ambavyo viliuzwa huko nyuma na kisha kutelekezwa.
  7. Kuboresha vivutio kwa ajili ya uwekezaji kwenye viwanda vitakavyotumia malighafi mbalimbali ziliopo nchini vikiwemo viwanda vya nguo, ngozi, usindikaji wa matunda, mbogamboga na usanifu wa madini ya vito.
  8. Kuendelea kuhamasisha uanzishaji na uimarishaji wa Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (SEZ).
  9. Kuendelea kutekeleza mkakati unganishi wa kufufua na kuendeleza viwanda vya ngozi.
  10. Kuandaa taarifa kuhusu fursa za uwekezaji katika miradi ya maendeleo ya viwanda nchini.

Kuhusu viwanda vidogo, Serikali itatekeleza yafuatayo:-

  1. Kuendeleza programu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini kwa kutoa ushauri, mafunzo, mitaji na huduma za kiufundi kwa wajasiriamali.
  2. Kuongeza mchango wa viwanda vidogo na biashara ndogo (SMEs) katika pato la Taifa kutoka asilimia 33 ya GDP hivi sasa kufikia asilimia 40 mwaka 2015.
  3. Kuendeleza, kuzalisha na kusambaza teknolojia za kuongeza thamani ya mazao kupitia vituo vya SIDO vilivyopo Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lindi, Iringa na Kigoma.
  4. Kutoa elimu na kuwajengea uwezo wakulima wa kusindika mazao kabla ya kuyauza kama vile usindikaji wa asali, utengenezaji wa mvinyo, utengenezaji wa juisi pamoja na ufungashaji wa bidhaa kwa kutumia teknolojia ya TBS.
  5. Kuwaunganisha wajasiriamali wadogo na makampuni makubwa yaliyotayari kununua bidhaa zao.
  6. Kujenga uwezo wa SIDO na kuwatafutia vyanzo vya fedha ili kuwawezesha kutoa mafunzo ya usindikaji kwa wajasiriamali wadogo. Aidha, Sheria iliyoanzisha SIDO itafanyiwa mapitio ili iendane na mahitaji ya uchumi wa sasa.
  7. Kuendeleza miundombinu ya viwanda vidogo na biashara ndogo.

Kuhusu biashara, Serikali itatekeleza yafuatayo:-

  1. Kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya ndani, kikanda na kimataifa, zikiwemo fursa za masoko ya AGOA, EBA, China, Japan, Canada na India ili kukuza biashara ya nje kwa kiwango kikubwa.
  2. Kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali kuhusu mbinu za kuyafikia masoko ya nje.
  3. Kuendelea na majadiliano ya ubia wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Ulaya (EU).
  4. Kuendelea na utekelezaji wa uanzishwaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendelea kutekeleza Itifaki ya Biashara ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
  5. Kufanya utafiti wa kina juu ya gharama za kufanya biashara nchini kwa lengo la kupunguza gharama hizo na kuchochea ukuaji wa biashara.

Kuhusu Mapinduzi ya kilimo, Serikali itatekeleza yafuatayo:-

  1. Kuanzisha vituo vitatu vya biashara vya kanda katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Arusha.
  2. Kuratibu na kuhamasisha ushiriki wa wajasiriamali wa Tanzania katika maonesho ya biashara ya kimataifa ndani na nje ya nchi.
  3. Kufanya utafiti wa masoko na bei ili kupanua wigo wa mahitaji ya masoko ya bidhaa zetu.
  4. Kuanzisha programu ya kuwa na utambulisho wa kitaifa kwa bidhaa.

Kuhusu masoko, Serikali itatekeleza yafuatayo:-

  1. Kukamilisha mkakati wa Sera ya Masoko na Bidhaa za Kilimo.
  2. Kuendeleza miundombinu ya masoko ya mikoa na kuanzisha masoko katika vituo vya mipakani ili kukuza biashara ya ndani na kikanda.
  3. Kutekeleza mkakati wa kukuza mauzo nje na mpango unganishi wa biashara.
  4. Kuendeleza biashara ya ndani ikiwa ni pamoja na kujenga dhana ya kutumia bidhaa zilizozalishwa Tanzania (NUNUA BIDHAA ZA TANZANIA).
  5. Kuboresha na kupanua wigo wa biashara mtandao katika ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
  6. Kuwalinda wajasiriamali wa ndani kwa kutoingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ambazo zinaua soko la ndani la bidhaa zao, kwa mfano samani.
  7. Kupanua matumizi ya simu za viganjani katika kutoa taarifa za bei ya mazao na masoko kwa wakati. Aidha, kuangalia uwezekano wa kuanzisha mbao za matangazo katika ngazi ya Wilaya na Mkoa ili kutoa taarifa mbalimbali ikiwemo bei na masoko kwa wakati muafaka.
  8. Kuendeleza mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara.
  9. Kuendeleza miundombinu ya masoko na kuanzisha masoko mipakani kama vile Karagwe, Kigoma, Holili, Horohoro, Namanga, Sumbawanga, Taveta na Tarakea.
  10. Kuendeleza utekelezaji wa Mfuko wa Stakabadhi za Mazao Ghalani.
  11. Kushirikiana na Sekta Binafsi katika kubuni na kutekeleza mikakati ya masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.
  12. Kuendeleza na kuboresha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na usambazaji wa taarifa za masoko.
  13. Kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa kutekeleza Sheria ya Usajili wa Shughuli za Biashara (BRELA).

Utekelezaji kamili wa malengo ya sehemu hizi nne za viwanda, biashara, Kilimo Kwanza na masoko unahitaji upatikanaji wa mitaji kwa wawekezaji na huduma za maji na umeme zisizo katikakatika mara kwa mara. Serikali itatakiwa kukabiliana na changamoto hizo kwa kasi na viwango stahiki.

Comments are closed.