Nishati na Madini
Katika miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya 2010 – 2015, Chama kitaitaka Serikali kuongeza kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka MW 1051 hadi MW 1722 (sawa na ongezeko la MW 671) na kupunguza ile ya tungamotaka kwa kuchukua hatua zifuatazo:-

Katika kipindi cha Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali iendelee kukuza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kwa kuchukua hatua zifuatazo:-

  1. Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liweze kushiriki katika umiliki wa migodi mikubwa na ya kati na katika utoaji huduma katika sekta ya madini na litumike kuwaendeleza wachimbaji wadogo.
  2. Kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya madini kwa kujenga uwezo wa Serikali katika usimamizi, uimarishaji wa miundombinu zikiwemo ofisi, vitendea kazi, kuongeza na kuwaendeleza wataalamu kwenye sekta ikiwa ni pamoja na kuimarisha wakala za Geological Survey of Tanzania (GST) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA).
  3. Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji, utafutaji, uchimbaji na uongezaji thamani katika madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa.
  4. Kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini, kuwarasimisha, kuwatafutia maeneo, kuwawezesha kupata mikopo na mitaji kwa kuanzisha mifuko maalumu, kuwapa mafunzo, teknolojia bora na maarifa. Aidha, katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanachangia katika uchumi wa nchi yatawekwa mazingira mazuri ya kuwawezesha kuendesha shughuli za madini kwa usalama na kutunza mazingira.
  5. Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya usalama, utunzaji wa mazingira na afya migodini.
  6. Kujenga uwezo wa utaalamu wa kushiriki kwa ukamilifu katika mikataba yote ya madini kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi.
  7. Kuandaa soko bora la ndani la kuuzia madini lililowazi ili madini yetu yasiuzwe kilanguzi nje ya nchi.
  8. Serikali kuwa na hisa katika uchimbaji mkubwa wa madini.
  9. Kuandaa mkakati wa uchimbaji wa madini ya “uranium” tuliyonayo ili yachangie katika modenaizesheni ya uchumi.
  10. Serikali ihakikishe kwamba migodi yote mikubwa inapata huduma zake kutoka hapa hapa nchini kama vile vyakula, ulinzi n.k.
  11. Kuongeza uwezo wa kitaalamu kwa Watanzania wanaojishughulisha katika Sekta ya Madini.

Katika miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya 2010 – 2015, Chama kitaitaka Serikali kuongeza kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka MW 1051 hadi MW 1722 (sawa na ongezeko la MW 671) na kupunguza ile ya tungamotaka kwa kuchukua hatua zifuatazo:-

  1. Kuboresha sera, sheria na kanuni zinazoongoza sekta ya nishati nchini.
  2. Kuunganisha gridi ya Tanzania na gridi za nchi jirani ili kuimarisha upatikaji wa umeme nchini.
  3. Kukamilisha upelekaji wa umeme kwenye Mikoa na Wilaya ambako gridi ya Taifa haijafika. Aidha, mkakati kabambe wa kupeleka umeme vijijini utaandaliwa na kutekelezwa kwa kumshirikisha Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  4. Kuimarisha mfuko wa nishati vijijini kwa kubuni vyanzo vya ziada vya kuchangia mfuko huu.
  5. Kuandaa na kutekeleza mpango utakaoipunguzia TANESCO baadhi ya majukumu na kuishirikisha sekta binafsi katika kuongeza na kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini. Uzalishaji wa umeme kwa kutumia rasilimaji za maji zilizopo utaendelea kuwa moja ya majukumu ya TANESCO.
  6. Kuendeleza na kupanua uzalishaji, usambazaji na matumizi ya gesi asilia; na
  7. Kuendeleza utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
  8. Kujenga mradi wa umeme wa Kinyerezi wenye uwezo wa MW 240.
  9. Kuendeleza mradi wa umeme wa Kiwira (MW 200) na Mchuchuma (MW 240), Ngaka (MW 200) vitakavyozalisha umeme unaotokana na makaa ya mawe.
  10. Kuanza utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme (358MW) kwa kutumia maji katika bonde la mto Ruhuji.
  11. Kuzalisha umeme (300MW) kutokana na gesi asili ya Mnazi Bay.
  12. Kupanua mitambo ya kusafisha gesi na bomba la kusafirisha gesi kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam.
  13. Kutekeleza mradi wa usambazaji wa gesi asili Dar es Salaam kukidhi mahitaji ya sekta mbalimbali.
  14. Kufanya tathmini na kujenga mfumo wa kusambaza gesi asilia nchini.
  15. Kuanza mchakato utakaowezesha utekelezaji wa mradi wa kufua umeme kwenye vyanzo vya maji katika maporomoko ya Stiegler’s Gorge, Ruhuji, Rumakali, Mpango, Nsovwe na Ruvuma.
  16. Kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta na bomba la kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza (1200 km).
  17. Kuongeza kasi ya uunganishwaji umeme kupitia mifumo nje ya gridi kwa kuhamisha matumizi ya nishati jadidifu kama umeme wa jua, upepo na tungamotaka kupitia mradi wa TEDAP.
  18. Kuandaa programu ya kupunguza matumizi ya umeme hususan viwandani na majumbani.
  19. Kufufua na kupanua mitambo ya TPDC ya kusafishia mafuta na kuhakikisha kwamba mitambo hiyo inafanya kazi wakati wote.
  20. Kuwa na mpango wa kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ya jua, upepo na fungamotaka (biogas).
  21. Kuanza utekelezaji wa njia Kuu ya Umeme ya Zambia, Tanzania na Kenya (ZTK) inayounganisha mitandao ya Umeme ya nchi za Mashariki ya Afrika na nchi za Kusini.
  22. Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa KV 132 wa Makambako-Songea utakaofikisha umeme wa gridi wilaya za Songea, Namtumbo, Mbinga, Nyasa na Ludewa.
  23. Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi ili iwekeze katika uzalishaji wa nishati mbadala kutokana na jua, upepo, biogas na vyanzo vingine kwa kiwango kikubwa na kuongeza uwezo wa usambazaji kwa gharama nafuu zaidi kwa njia ya ubia wa sekta ya Umeme na Sekta binafsi (PPP).
  24. Kuongeza uwezo wa gridi ya Taifa toka MW 240 hadi MW 400.

Comments are closed.