Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya miaka ya 2010 – 2015, Chama kitaielekeza Serikali kuyalinda na kuyaendeleza mafanikio kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
(a) Kuimarisha Mfuko wa Barabara (Tanzania Road Fund) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Barabara kwa kufanya yafuatayo:-
- Kubuni na kupanua wigo wa vyanzo vya mfuko wa barabara ili kuongeza kiwango cha Mfuko.
- Kuandaa mkakati endelevu wa kukarabati barabara na madaraja nchini ili kuinua uhai wa miundombinu hiyo na kupunguza kwa kiwango kikubwa gharama za kuzikarabati.
(b) Kutenga fedha za maendeleo ya barabara za miji ikiwemo Dar es Salaam, Arusha na Mwanza na kuangalia uwezekano wa kuunda chombo maalumu cha kusimamia na kuendeleza ujenzi wa barabara za mijini.
(c) Kukamilisha ukarabati wa barabara zote ambao unaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami ambao umekwisha anza katika Barabara Kuu na Barabara za Mikoa kama ifuatavyo:
- Manyoni – Isuna (Km 54);
- Kagoma – Biharamulo – Lusahunga (Km 154);
- Ndundu – Somanga (Km 60);
- Sumbawanga – Matai – Kasanga (Km 112);
- Marangu – Tarakea – Rongai – Kamwanga (Km 98);
- Minjingu – Babati – Singida (Km 222);
- Korogwe – Handeni (Km 65);
- Mziha – Turiani – Magole (Km 84.6)
- Dumila – Kilosa (Km 63)
- Bariadi – Lamadi (Km 71.8);
- Mbeya – Chunya – Makongolosi (Km 115);
- Tanga – Horohoro (Km 65);
- Masasi – Mangaka (Km 54);
- Makofia – Msata (km 64);
- Mwandiga – Manyovu (km 60);
- Handeni – Mkata (km 54);
- Kisarawe – Maneromango (Km 54);
- Njombe – Makete (Km 109).
- Barabara ya Kilwa/DSM (km 12);
- Barabara ya Mandela (km 16);
- Msimba – Ikokoto – Mafinga (Km 219);
- Arusha – Namanga (Km 105);
- Chalinze – Segera – Tanga (Km 245); na
- Isaka – Lusahunga (km 242)
- Kwasadala-Masama (Km 12.2);
- KiboshoShine-Kwa Raphael-International School (Km 43);
- RauMadukani-Mawela-UruNjari (Km 12.5);
- KiruaNduoni-Marangu Mtoni (Km 31.5);
- Kahama Mjini (Km 5).
(d) Kuanza Ujenzi mpya na ukarabati kwa Kiwango cha Lami Barabara zifuatazo:
- Bunda – Kisorya – Nansio (Km 93);
- Tunduma – Sumbawanga (Km 230);
- Rujewa – Madibira – Mafinga (Km 151);
- Babati – Dodoma – Iringa (Km 523);
- Sumbawanga – Kanyani – Nyakanazi (Km 562);
- Nata – Fort Ikoma (Km 141);
- Nzega – Tabora (Km 116);
- Manyoni – Itigi – Tabora (Km 264);
- Ipole – Koga – Mpanda (Km 255);
- Makurunge – Saadani – Pangani – Tanga (Km 178);
- Matai – Kasesya (Km 65);
- Mangaka – Mtambaswala (Km 65);
- Mto wa Mbu – Loliondo – Mugumu – Nata – Makutano (Km 452);
- Kyaka – Bugene (km 59);
- Mbinga – Mbamba bay (Km 66);
- Tunduru – Namtumbo (Km 194);
- Kamwanga – Sanya Juu (Km 75);
- Tabora – Urambo (Km 90);
- Uvinza – Kidahwe (Km 77);
- Daraja la Malagarasi na barabara zake (Km 48);
- Uyovu – Bwanga – Biharamuro (Km 112);
- Kisesa –Usagara (Km 17);
- Namtumbo – Songea (Km 70);
- Peramiho – Mbinga (Km 78);
- Kawawa Jct – Mwenge – Tegeta (Km 17);
- Segera – Same – Himo (km 261);
- Makambako – Songea (km 295);
- Mtwara – Masasi (km 200);
- Arusha – Moshi – Himo – Holili (km140);
- Arusha – Minjingu (km 104);
- Nyanguge – Musoma – Sirari (km 262); na
- Sanya Juu – Bomang’omba (Km 25).
Kuzifanyia Upembuzi na Usanifu Barabara Zifuatazo:-
- Tabora – Mambali – Bukene – Itobo – Kahama (Km 149);
- Lupilo – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Kitanda (km 396);
- Ifakara – Mahenge ( Km 67);
- Kibondo – Mabamba (km 35);
- Kolandoto- Lalago – Mwanhuzi – Matala – Oldeani Jct (km 328);
- Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105);
- Mpemba – Isongole (Tanzania/Malawi) (km 49);
- Soni – Bumbuli –Dindira – Korogwe (km 74);
- Makofia – Mlandizi – Vikumburu (Km 148);
- Kibaoni – Majimoto – Inyonga Km 162);
- Mpanda- Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama (km 428);
- Makongolosi- Rungwa – Mkiwa (km 412);
- Mtwara – Newala – Masasi (km 209);
- Handeni – Kiberashi – Kondoa – Singida (Km 460);
- Kibaha – Mapinga (Km 23);
- Geita-Bukoli-Kahama (Km 107);
- Mbande-Kongwa Jct – Mpwapwa (Km 50).
Vivuko
Kuandaa utaratibu wa kununua vivuko vipya vyenye uwezo wa kubeba tani 50 kila kimoja kwa ajili ya maeneo yafuatayo:-
(a) Msanga Mkuu (Mtwara)
(b) Rusumo (Kagera)
(c) Itungi Port – Matema (Kyera)
(d) Kilambo (Mtwara) kitakachotoa huduma kati ya Tanzania na Msumbiji.
Madaraja
(a) Kuanza ujenzi wa daraja la mto Kilombero na daraja la mto Mwatisi katika mkoa wa Morogoro.
(b) Kuanza ujenzi wa daraja la Malagarasi, Kigoma.
(c) Kukamilisha maandalizi na kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kuunganisha Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam.
(d) Kuanza ujenzi wa daraja la Nangoo (Mtwara), Sibiti (Singida), Ruhekei(Mbinga) na Mbutu (Igunga).
(e) Kuanza usanifu wa daraja la Ruhuhu (Ruvuma).
Usafiri na Uchukuzi
(a) Kuendelea kuiimarisha Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kwa lengo la kuipa uwezo wa kutoa huduma bora kwa kusafirisha abiria na mizigo ya ndani na nchi jirani. Pia, reli itaendelezwa kama mhimili wa mpango wa maendeleo wa eneo la Ukanda wa kati.
(b) Kushirikiana na Serikali za Rwanda na Burundi, kuanza ujenzi wa reli mpya kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali (Rwanda) na Msongati (Burundi).
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuboresha miundombinu ya reli na kuendeleza juhudi za kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa shirika kwa lengo la kuboresha huduma za abiria na mizigo.
(d) Kujenga na kuimarisha miundombinu ya Reli na Bandari kwa kukamilisha mtandao wa reli na kuunganisha bandari ya Tanga na reli ya Arusha -
Musoma:-
(i) Ujenzi wa bandari mpya eneo la Mwambani (Tanga),
(ii) kuboresha reli ya Tanga – Arusha,
(iii) kujenga reli mpya kati ya Arusha na Musoma,
(iv) Kuboresha bandari ya Musoma.
(e) Kuanza ujenzi wa reli ukanda wa Mtwara kwa kuchukua hatua za maandalizi ya mradi wa ujenzi wa reli ya Mtwara – Mchuchuma – Liganga.
(f) Kuendeleza huduma za uchukuzi kwenye maziwa kwa kuimarisha bandari za Kigoma, MbambaBay, Mwanza, Bukoba na Nansio.
(g) Kuboresha huduma za uchukuzi katika Bandari za Mwambao :
(i) Kupanua bandari ya Dar es Salaam na Mtwara
(ii) Kujenga bandari mpya Bagamoyo
(iii) Kujenga magati katika bandari za Mafia na Lindi.
(h) Kutekeleza Programu ya Uwekezaji Katika Sekta ya Uchukuzi kwa kuvutia wawekezaji binafsi katika uendeshaji wa sekta ya uchukuzi kwa kuzingatia Sera ya Sheria ya ushirikishaji wa sekta binafsi (PPP).
(i) Kuimarisha usafiri wa anga iIi uchangie kwenye pato la Taifa kwa kuchukua hatua zifuatazo:
(i) Kuimarisha na kuboresha kiwanja cha JNIA kwa kujenga jengo jipya la abiria na majengo mengine ya huduma za abiria.
(ii) Kukamilisha na kutekeleza Mpango Kabambe wa Usafiri wa Anga.
(iii) Kukamilisha ujenzi wa kiwanja kipya cha Kimataifa cha ndege cha Songwe (Mbeya)
(iv) Kuanza ujenzi wa kiwanja kipya cha Kimataifa cha ndege cha Msalato (Dodoma).
(v) Kufanyia upembuzi na usanifu kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Bagamoyo.
(vi) Kukamilisha uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Mwanza na Mtwara.
(vii) Kukamilisha uboreshaji wa viwanja vya ndege vya Mafia, Arusha, Mpanda, Sumbawanga Bukoba, Kigoma, Tabora na Shinyanga.
(viii) Kuunda upya Shirika la Ndege la Taifa kwa kushirikisha sekta binafsi.
(j) Kupunguza Msongamano wa Magari katika Jiji la Dar es Salaam kwa kufanya yafuatayo:
(i) Kujenga barabara za juu (fly overs) kwenye makutano ya barabara maeneo ya Ubungo na TAZARA,
(ii) Kupanua mtandao wa barabara za Jiji za Dar es Salaam kwa kujenga na kukarabati barabara zifuatazo:-
- Mbezi (Morogoro road)-Malambamawili-Kinyerezi-Banana (Km 14.0);
- Tegeta Kibaoni-Wazo-Goba-Mbezi Mwisho (Km 20.0);
- Tangi Bovu-Goba (Km 9.0);
- Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni (Km 2.6);
- Kimara-Kilungule-External Mandela road (Km 9.0);
- Ubungo Bus Termanial-Mabibo-Kigogo Round about (Km 6.4);
- Kigogo Round About-Bonde la Msimbazi-Twiga/Msimbazi Junction (Km 2.7);
- Tabata Dampo-Kigogo- Ubungo Maziwa External (Km 2.25);
- Old Bagamoyo-Garden Road (Km 9.1); na
- Jet Corner-Vituka-Devis Corner (Km 6.0).

