Viwanda, Biashara na Masoko
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia 15 mwaka 2015 kwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta za viwanda, biashara na masoko kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

Kuongozeka kwa fursa za masoko nafuu baina ya Nchi na Nchi, Kikanda na ya Kimataifa: Serikali imeendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kutumia fursa za masoko zilizopo kukuza biashara ikiwa ni pamoja na soko la SADC, EAC, WTO na masoko ya upendeleo maalumu katika nchi mbalimbali kama vile China, Japani, Korea Kusini, India, EU (EBA), Marekani (AGOA).

  • Fursa za masoko zimeiwezesha Tanzania kuongeza mauzo nje kutoka Shilingi milioni 1,871,265 mwaka 2005 hadi Shilingi milioni 3,220,495.7 mwaka 2008.
  • Nchi wanachama wa SADC ikiwamo Tanzania zimeendelea kutekeleza makubaliano yaliyomo kwenye itifaki ya biashara SADC ikiwa ni pamoja na kupunguziana viwango vya ushuru wa bidhaa.
  • Tanzania imetekeleza itifaki hiyo na ikazindua Eneo Huru la Biashara SADC (SADC Free Trade Area) Agosti, 2008.
  • Programu ya Uuzaji Bidhaa Nchi za Nje (Export Development Strategy) inaendelea kukua na kuimarishwa ambapo wafanyabiashara na wawekezaji 405 kutoka jimbo la Guangdong – China walifanya makubaliano ya uwekezaji na biashara nyenye thamani ya Dola za Kimarikani milioni 54.8.

2. Uendelezaji wa Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya nje (EPZ): Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kwa kuanzisha Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ.  Wawekezaji     wamehamasishwa kuja kujenga viwanda na kuzalisha kwa ajili ya kuuza nje ya nchi. 

  • Kuanzia mwaka 2006 hadi 2008, jumla ya viwanda 46 vimesajiliwa chini ya mpango wa EPZ, vikiwemo 18 vya kujenga miundombinu ya EPZ na 28 ni viwanda vya uzalishaji.  Viwanda ambavyo vimeanza uzalishaji ni pamoja na: Cami Apparel Ltd. Unnats Fruts Processing Ltd, Kibo Trade Textile Ltd, Nethealth Ltd.  Na Honey Care Tanzania Ltd.
  • Mamlaka ya EPZ kwa kushirikiana na uongozi wa Mikoa wamebainisha na kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya EPZ na SEZ yenye kubwa wa hekta 2,000 kwa kila mkoa katika mikoa 14 ambayo ni Pwani, Tanga, Arusha, Manyara, Mwanza, Mara, Kagera, Kigoma, Mtwara, Ruvuma, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na Lindi.
  • Mamlaka ya EPZ imeanza kuhamasisha wawekezaji wa kujenga viwanda katika eneo la Benjamini William Mkapa SEZ (BWM-SEZ) Mabibo, DSM na tayari wawekezaji 24 wamewasilisha maombi ya kuwekeza katika eneo hilo.  Wawekezaji 5 wameishapewa leseni na kujenga viwanda katika eneo hilo.
  • Viwanda 18 kupitia EPZ vimeanzishwa ambapo jumla ya Dola za Marekani zaidi ya 150 million zimewekezwa. Kutokana na ukarabati pamoja na uwekezaji, mchango wa bidhaa za viwandani katika mauzo nje umeongezeka kutoka asilimia 9.3 mwaka 2005 na kufikia asilimia 14.5 mwaka 2007. Ajira imeongezeka  kutoka wafanyakazi 89,316 mwaka 2005 nakufikia wafanyakazi 110,586 mwaka 2008.

3.Kuongezeka kwa malipo anayopata mkulima wa zao la Korosho kupitia matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Mazao ghalani: Mfumo wa stakabadhi za Maghala ulianzishwa nchini kisheria mwaka 2005 baada ya Bunge kupitisha Sheria Namba 10 ya mwaka 2005 na kanuni zake mwaka 2006.

  • Mkulima kupata bei nzuri kutoka sh 400/kilo kabla ya mfumo mwaka 2005/2006 hadi sh 610/ kilo mwaka 2007/08 na Sh 1,000 kwa kilo mwaka 2009/2010.
  • Wakulima wamepata malipo ya tatu (maarufu kama malipo ya majaliwa) katika mwaka 2006/2007 sh 175/- kwa kilo na msimu wa 2009/2010 malipo haya yamepanda hadi sh 300/- kwa kilo.
  • Wakulima kupitia mfumo huu sasa wanauza mazao yao kupitia vipimo sahihi (Kilo) na kuachana na vipimo vinavyomnyonya mkulima (Mfano Kangomba)
  • Mfumo umefanikiwa kuondoa walanguzi (Middlemen) ambao walikuwa wakinunua zao la korosho kwa bei ndogo sana
  • Mfumo umewezesha Taasisi za fedha CRDB na NMB kujihusisha na ununuzi wa zao hilo kupitia vyama vya ushirika wa  mazao
  • Kuongezeka kwa ubora wa korosho kutokana na mfumo wa kuuza kwa kuzingatia madaraja (Grades of products)

4. Ukuaji wa mchango wa Sekta ya Viwanda katika pato la taifa na uanzishwaji na uongezwaji wa uwezo wa uzalishaji wa Viwanda  vya Nguo, Mbolea, Saruji, Chuma na Kemikali: Ufanisi katika sekta ya Viwanda umeongezeka, na hivyo ukuaji wa sekta umeongezeka na kufikia asilimia 9.9 mwaka 2008 kutoka asilimia 9.6  mwaka 2005.

  • Mchango wa sekta katika pato la Taifa (GDP)   umeongezeka kutoka asilimia 8.9 mwaka 2005 hadi asilimia 9.4 mwaka  2008.
  • Utumiaji wa uwezo (capacity Utilization) umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 30 mwaka 2005/2006  hadi wastani wa asilimia 50 mwaka 2008/2009.
  • Mchango wa bidha za viwandani katika mauzo  nje umeongezeka kutoka asilimia 9.31 mwaka 2005 hadi asilimia 14.5 mwaka 2007 na  kupungua kidogo hadi asilimia 13.6 mwaka 2008.
  • Ajira katika sekta ya Viwanda imeongezeka kutoka 89,316 mwaka 2005 hadi 92,015 mwaka 2008.
  • Kuongezeka kwa utumiaji wa uwezo  (capacity utilization) kutoka asilimia 31 mwaka 2006 na kufikia wastani wa asilimia 51 mwaka 2008. Aidha vipo baadhi ya viwanda ambavyo utumiaji wa uwezo ni zaidi ya asilimia 80; kwa mfano viwanda vya saruji, bia, sigara
  • Katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2009, viwanda sita (6) vya kusindika ngozi vyaenye uwezo wa kusindika ngozi ghafi zadi ya futi za mraba milioni 54.32 kwa mwaka vinaendelea na shughuli za usindikaji wa ngozi.
  • Viwanda hivyo ni Himo Tanneries (Moshi), Moshi Leather       Industries (Moshi), East Hides (T) LTD (Morogoro), Lake Trading Co. LTD         (Kibaha- Pwani), Salex Tanneries Ltd (Arusha) na Afro Leather       Industries Ltd (Dar es Salaam)
  • Kuongezeka kwa uwezo wa viwanda vya kusindika ngozi kutoka futi za mraba 6,038,000, sawa na asilimia 25.5 hadi futi za mraba 37,305,215 sawa na asilimia 72.2 mwaka 2009.
  • Kuongezeka kwa mauzo ya nje kwa ngozi zilizosindikwa na bidhaa za ngozi kutoka thamani Shilingi milioni 3,516,900 mwaka 2005 hadi shilingi milioni 13, 621,000 mwaka 2009
  • Kuongezeka kwa ajira katika sekta ya ngozi kutoka 280 mwaka 2005 hadi 520 mwaka 2009
  • Kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya nguo kutoka mita za mraba milioni 99.1 mwaka 2005 na kufikia mita za mraba milioni 150 mwaka 2009
  • Matumizi ya uwezo yameongezeka kutoka asilimia 30 mwaka 2005 hadi asilimia 50 mwaka 2008. Aidha, matumizi ya pamba ghafi yameongezeka kutoka tani 24,859 mwaka 2005 hadi tani 33,226 mwaka 2009.
  • Sekta ya nguo imeongeza ajira kutoka 10,073 mwaka 2005 hadi 18,000 mwaka 2009.
  • Mauzo ya nje kutoka Sekta ya nguo yameongezeka kutoka  shilingi bilioni 171.5 hadi shilingi bilioni 306.5 mwaka 2008
  • Uwezo wa kuzalisha Saruji umeongezeka kutoka tani 4,450,000 mwaka 2005 hadi tani 3,000,000 kwa mwajka baada ya kiwanda cha Tanzania Portland Cement Co. Ltd kuongeza ‘kiln’ yenye uwezo wa kuzalisha tani 700,000 kwa mwaka na pia Kiwanda cha Tanga Cement Co. Ltd kimesimika mtambo wa kusaga “clinker” wenye uwezo wa kuzalisha tani 500,000 za saruji kwa mwaka.
  • Kuongezeka kwa viwanda vya kuyeyusha vyuma kutoka viwanda 8 mwaka 2005 hadi kufikia 20 mwaka 2009. Viwanda hivi vinauwezo wa kuzalisha tani zaidi ya 600,000 za nondo kwa mwaka.
  • Kuongezeka kwa ajira katika viwanda vya kuyeyusha chuma kutoka 670 mwaka 2005 hadi 1,050 mwaka 2009

5. Uanzishwaji Na uimarishaji WA miundo mbinu ya masoko ya mipakani mfano Sirari, Mutukula, Shirati na Mirongo pamoja na uanzishwaji wa Vituo vya pamoja vya mpakani. Mfano kati ya Tanzania na Zambia (Miji ya Tunduma-Tanzania na Nakonde-Zambia): Masoko ya mipakani ni muhimu sana kwa Taifa kwa kuwa ni kichocheo kikubwa cha ongezeko la Pato la Taifa na ukuaji wa Uchumi, hasa katika kipindi ambacho Tanzania inajiandaa kuingia katika soko la pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki, na utekelezaji wa Mpango Unganishi wa Biashara (Tanzania Trade Intergration Strategy – TTIS).

  • Kuiunganisha mikoa ya mipakani mwa Tanzania na nchi jirani, nchi hizo ni Malawi, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Zambia n anchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  • Kuziwezesha nchi za jirani kutumia bandari zetu za Mtwara, Tanga  na Dar es Salaam hatua inyofungua biashara na kuongeza mapato kupitia njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kodi, manunuzi ya bidhaa na huduma wanazotumia wafanyabiashara wanapokuwa hapa nchini.
  • Kupunguza urasimu na upotevu wa rasilimali muda katika ufanyaji biashara
  • Kuongezeka kwa fursa za masoko kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa mikoa ya mipakani
  • Kuondokana na kero ya upungufu wa bidhaa muhimu kwa wananchi mfano Sukari ya ndani inayopelekwa katika mikoa Mtwara na Ruvuma imebainishwa kuwa ni kidogo sana, ifikapo haiuziki kutokana na ushindani wa bei na sukari kutoka nchini Malawi na Msumbiji (Sukari inayozalishwa na Viwanda vya Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar Company, TPC Moshi na Kagera Sugar ni takriban Tani 258,420 kwa mwaka ikilinganishwa na mahitaji ya Tani 350,000 kwa nchi nzima kwa mwaka).

Kupata bidhaa kwa urahisi na bei nafuu mfano  Sukari mkoani Mtwara inauzwa Tsh 1700/- hadi 2000/- wakati Msumbiji sukari ni Tsh 1500/- hadi 1800/- na Mkoani Ruvuma bei ya sukari ni Tsh 1800/- hadi 2000/- wakati Malawi bei ya sukari ni Tsh 1200/- hadi 1400/

Comments are closed.