Utawala Bora
Serikali ya awamu ya nne ni muumini thabiti wa dhana za demokrasia na utawala bora ambazo misingi yake ni madaraka ya wananchi, utawala wa sheria uwabikaji na uadilifu. (vita dhidi ya rushwa)

Katika kuzidi kuimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora katika kipindi cha 2005-2010, Serikali ya awamu ya nne imehakikisha utekelezaji wa mambo yafuatayo;

1.Serikali ya Awamu ya Nne imehakikisha kuwa Amani, Utulivu na Umoja wa nchi yetu na watu wake vinadumishwa;

2.Serikali ya Awamu ya Nne imedumisha na kuendeleza mafaniko yaliyopatikana tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo;

3.Serikali ya Awamu ya Nne imeendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kazi mpya;

4.Serikali ya Awamu ya Nne imetimiza ipasavyo wajibu wake wa utawala na maendeleo, na itaendesha dola kwa misingi ya utawala bora na uwajibikaji; utawala wa sheria unaoheshimu na kulinda haki za binadamu; itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa bila ya woga wala kuoneana muhali.

5.Serikali ya Awamu ya Nne imeimarisha uwezo wake wa kulinda maisha na mali za raia wake.  Itapambana na uhalifu wa kila aina, na majambazi hayataachwa yatambe yatakavyo;

6.Serikali ya Awamu ya Nne imehakikisha mipaka ya nchi yetu ipo salama.  Haitamruhusu mtu au nchi yeyote kuchezea mipaka ya nchi yetu na uhuru wetu;

7. Serikali ya Awamu ya Nne imefanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa Tanzania ina mahusiano mazuri na mataifa yote duniani, pamoja na mashirika ya kimataifa na kikanda;

8.Serikali ya Awamu ya Nne imejali sana maslahi na mahitaji ya makundi maalum katika jamii kama vile wanawake, vijana, watoto, wazee, walemavu na yatima;

9.Serikali ya Awamu ya Nne imeongoza mapambano mapya ya kuhifadhi mazingira ili vizazi vijavyo virithi nchi nzuri, na shughuli za utamaduni na burudani;

10.  Serikali ya Awamu ya Nne imeendeleza michezo, na shughuli za utamaduni na burudani.

Comments are closed.