Katika kipindi cha 2005-2010, msistizo katika uhusiano wa wa kimataifa ilikuwa katika kuendeleza Diplomasia ya Uchumi. Ofisi zetu za Ubalozi zimemarishwa kiutalaamu na hatua zimechukuliwa kuhakikisha
Kuendeleza sera ya ujirani mwema na kushiriki katika kuleta amani na usalama katika nchi za Afrika na duniani kwa ujumla. Baadhi ya mafanikio hayo yanaonekana nchini Burundi, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tanzania inatoa mchango pia katika juhudi za amani nchini Sudan.
Kulitangaza jina la nchi yetu na kuitetea heshima yake miongoni mwa mataifa. Wizara kupitia balozi zake na majukwaa ya kimataifa imefanikiwa kuijengea heshima mbele ya jamii ya kimataifa. Kwa mfano Tanzania kutembelewa na viongozi wa mataifa makubwa kama vile China, Marekani na viongozi wa Mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa. Aidha, Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutan wa Jukwaa la Uchumi kwa Afrika (World Economic Forum for Africa) utakaofanyika mwezi Mei, 2010.
Kuendelea kuiletea nchi yetu maslahi ya kiuchumi kwa kuwavutia wawekezaji wenye mitaji, teknolojia ya kisasa na kukuza biashara na kuvutia watalii; kwa mfano; Mkataba wa Maendeleo ya Milenia (Millenium Challenge Compact) ambapo Marekani itaipatia Tanzania dola za Kimarekani milioni 698 kwa kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kuimarisha miundombinu husussan barabara, umeme na huduma za kijamii kama vile maji na afya. Serikali ya China imeahidi kufufua miradi ya ushirikiano hususan Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Nguo cha Urafiki n.k. Katika kukuza utaii Shirika la Ndege la Qatar lilianzisha safari za ndege kati ya Doha na Dar es Salaam mwaka 2007.
Kushiriki katika kuimarisha Jumuiya za kimataifa na za kikanda. Mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika mashirika ya kimataifa na kikanda ni pamoja na kuchaguliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 2008, kuteuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Asha-Rose Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Tanzania kuchaguliwa kuwa Makao Makuu ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu n.k.
Kuitambua Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Ughaibuni (Tanzanians in the Diaspora) na kuweka utaratibu utakaowezesha kuchangia maendeleo ya Taifa lao. Wizara ipo katika mchakato wa kuanzisha Idara itakayoratibu na kushughulikia Watanzania walioko ughaibuni.

