Uchumi
Mkakati mmojawapo, ambao tayari tunashughulika, ni wa kutambua rasmi rasilimali na biashara za wanyonge ambazo bado ziko kwenye sekta isiyo rasmi ili zitumike kuwafanya wawe washiriki kamili kwenye uchumi rasmi wa taifa"

1. USIMAMIZI WA UCHUMI JUMLA: Ukuaji wa Uchumi Katika kipindi cha miaka minne (2005 – 2009). Uchumi umeendelea kuimarika na Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.2 kwa mwaka katika kipindi hicho. Ukuaji huu wa uchumi ulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika sekta za: Bidhaa za viwanda; ujenzi; fedha; na mawasiliano na uchukuzi.

2. Pato la Mtanzania; Pato la Mtanzania limekuwa likiongezeka katika kipindi chote cha awamu ya nne kutoka Dola za Kimarekani 392.8 mwaka 2005 hadi dola 525.2 mwaka 2008.

3.Mwenendo wa Riba; viwango vya riba vimeonesha mwelekeo mzuri hasa

kuanzia mwaka wa fedha 2006/07, ambapo riba kwenye amana za akiba zimekuwa zikiongezeka, wakati riba zinazotozwa kwenye mikopo zimekuwa zikipungua. Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2009/10 wastani wa

viwango vya riba kwa amana za akiba za muda mfupi (hadi mwaka mmoja)ulikuwa asilimia 8.92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.21 katika mwaka wa fedha 2003/04. Katika kipindi hicho, wastani wa viwango vya riba vilivyotozwa na benki za biashara kwa mikopo ya mwaka mmoja ulipungua hadi asilimia 13.93 kutoka asilimia 15.75. Kutokana na mwelekeo huo wa riba, tofauti kati ya viwango vya riba kwenye amana za mwaka mmoja na viwango vya riba kwenye mikopo ya mwaka mmoja ilishuka kutoka 10.54 mwaka 2003/04 hadi 5.01mwaka 2009/10, sawa na kushuka kwa asilimia 47.5.

4. Biashara ya Bidhaa Nje; Mauzo ya bidhaa nje yaliongezeka kwa asilimia 3.2 hadi kufikia dola za Kimarekani 2,697.6 milioni mwezi Novemba 2009. Ongezeko hilo lilichangiwa na mauzo ya dhahabu kwa asilimia 9.0 hadi kufikia dola 1,023.8 milioni, tumbaku kwa asilimia 35.3 hadi kufikia dola 151.4. Aidha, mauzo ya kahawa nje yaliongezeka hadi kufikia dola 117.2 milioni, sawa na asilimia 29.0.

5.MAPATO YA NDANI; Katika kipindi cha miaka minne, Wizara ya Fedha na Uchumi, kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanya marekebisho ya mifumo na viwango vya baadhi ya kodi. Hatua hii imesaidia kuweka mazingira mazuri zaidi ya uzalishaji kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Aidha, wigo wa kodi umeongezeka katika kipindi hicho.

6.KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MIKOPO; Mikopo iliyotolewa na mabenki kwa sekta binafsi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi iliongezeka kutoka shilingi bilioni 1,571.0 mwezi Desemba 2005 hadi shilingi bilioni 4,710.2 mwezi Juni 2009, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 34.5 kwa mwaka. Mwezi Oktoba 2009 mikopo hiyo ilikuwa imefikia shilingi bilioni 4,836.0. Aidha, wastani wa riba kwa dhamana zote ilishuka kutoka asilimia 16.4,

7.KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI; Mifuko ya Dhamana ya Mikopo (Credit Guarantee Scheme): Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dhamana wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME Credit Guarantee Scheme) ambao unaratibiwa na Benki Kuu kumeboresha mazingira ya wenye mitaji midogo na ya kati waweze kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha. Tangu mfuko huu uanzishwe, jumla ya SMEs 48 zimepata udhamini wa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.054. Kati ya wajasiliamali hao, sekta ya uzalishiji inaongoza ikifuatiwa na sekta za ujenzi na kilimo. Ili kuleta ufanisi zaidi, mwaka huu Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10 kuongeza mtaji wa mfuko wa wajasiliamali wadogo na wa kati. Kuongeza fedha katika  Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK) kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5 zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.

Comments are closed.