![]()
Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya NISHATI ni pamoja na:-
- Kufungamanishwa kwa sekta ya nishati na uchumi na kuiweka sekta kwenye sekta za vipaumbele;
- Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Songo Songo na kuanza kutumia gesi asili kama chanzo cha nishati, hususan kwa kuzalisha umeme, viwandani na matumizi kwenye magari;
- Mikoa ya Mtwara na Lindi kupata umeme wa uhakika unaozalishwa kwa gesi asili ya Mnazi Bay;
- Kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji umeme nchini kwa MW 505 kutoka kwenye miradi ya Kihansi MW 180, Songas MW 180, Ubungo MW 100 na Tegeta MW 45;
- Kuongezeka kwa kasi ya utafutaji mafuta kulikopelekea ugunduzi wa gesi asili maeneo ya Mkuranga na Kiliwani Kaskazini (Kilwa);
- Kukamilika kwa miradi ya upelekaji umeme katika makao makuu ya wilaya za Serengeti, Ludewa, Mbinga, Simanjiro, Kilolo, Bahi, na Mkinga;
- Kukamilika kwa Sheria ya Nishati Vijijini na kuanzishwa kwa Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini;
- Kuandaliwa kwa Sheria za Umeme na Biashara ya Mafuta;
- Kukumilika kwa durusu ya Sera ya Taifa ya Nishati;
- Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji;
- Sekta binafsi kushiriki kwenye uwekezaji katika miradi ya umeme vijijini; na
- Kuweka mfumo wa mikopo ya muda mrefu kwa waendelezaji wadogo wa nishati vijijini.
- kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano kati ya African Development Bank [ADB] na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kugharimia mradi wa upelekaji umeme Bukombe na Longido;
- kukamilika kwa maandalizi ya kutekeleza miradi ya umeme wa jua katika mikoa ya Rukwa, Kigoma, Ruvuma, Shinyanga, Mtwara, Mbeya, Kagera na Tabora chini ya mradi wa Tanzania Energy Development and Access Expansion Program – TEDAP;
- kukamilika kwa utafiti wa kuangalia mienendo ya upepo katika maeneo ya Karatu (Arusha), Mkumbara (Tanga), Kititimo (Singida), Mgagao (Kilimanjaro) na Makambako (Iringa) vyenye uwezo wa kuzalisha umeme kati ya MW 50 – 150;
- Kukamilika kwa Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme (Power System Master Plan – PSMP, 2009 – 2033);na
- Kuwekwa kwa mazingira wezeshi kwa wazalishaji wadogo wa umeme kwa kutumia Standardized Small Power Purchase Agreement (SSPPA) ili kurahisisha na kuharakisha majadiliano na TANESCO kuhusu mauziano ya umeme.
Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya MADINI ni pamoja na:-
- Kuanzishwa kwa migodi saba katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2010. Migodi hiyo ni Bulyanhulu Gold Mine (2001); Geita Gold Mine (2000), North Mara Gold Mine (2002); TanzaniteOne Tanzanite Mine; Buganika Diamond Mine (2003); Tulawaka Gold Mine (2005); na Buzwagi Gold Mine (2009).
- Kuongezeka kwa uzalishaji wa madini kutoka kwenye migodi mikubwa na midogo na hivyo kuongeza kwa mapato ya Serikali kutokana na uchimbaji wa madini.
- Utafutaji wa madini umeongezeka ambapo zaidi ya leseni 3000 za utafutaji mkubwa wa madini zimetolewa, ukiwemo utafutaji wa madini ya urani.
- Wakala wa kukagua uwekezaji katika migodi mikubwa umeanzishwa na kuimarishwa.
- Serikali iliwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwapa leseni za uchimbaji mdogo (primary mining licences); kuwahamasisha waunde vikundi vya ushirika ili kuweza kuwasaidia vizuri zaidi.
- Wachimbaji wadogo wametafutiwa maeneo ya uchimbaji mdogo wa madini na kupewa huduma za ugani pamoja na kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali, uchimbaji salama, biashara ya madini, na namna ya kutafuta masoko.
- Kituo cha mafunzo kwa wachimbaji wadogo kimeanzishwa ili kuwasogezea huduma za ugani na mafunzo.
- Kuimarisha na kuwahamasisha wachimbaji wadogo washirikiane na wawekezaji wakubwa.
Sera Mpya ya Madini imeandaliwa na kupitishwa na Serikali 2009 na Sheria Mpya ya Madini 2010 inakamilishwa.




