1. Ujenzi wa barabara zilizoahidiwa mwaka 2005 umekamilka zikiwemo, Manyoni -Dodoma, Manyoni -Singida, na Mkurang -kibiti
2. Tumejenga vivuko vya uhakika kigamboni, MV Misungwi, MV Pangani, MV Kome
3. Tumejenga kiwanja cha ndege kipya cha Mbeya (Songwe) na tumeendelea kuimarisha viwanja vitano vya ndege (JNIA, Arusha, Mwanza, Kigoma na Mafia)
4. Tumejenga madaraja makubwa nchini kama lile la Mpiji, mchakato umeanza wa daraja la kigamboni Dar es salaam, Daraja la Kilombero mkoani Morogoro, usanifu wa daraja jipya la Ruvu na tumeanza ujenzi wa daraja la umoja baina ya Tanzania na Msumbiji.
5. Tuliahidi kuanza ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami kama ifuatavyo:
Barabara ya Tunduma –Sumbawanga ujenzi umeanza
Marangu-Tarakea-Songao ujenzi umekamilika
Minjigu-Babati-Singida – ujenzi unaendelea
Mbeya-Chunya-Makongolosi – ujenzi unaendelea
Arusha-Namanga – ujenzi unaendelea
Tanga-Horohoro –ujenzi unaendelea
Ukarabati za Barabara za Kilwa, Sam Nujoma na Nelson Mandela ama umekamilika ama unakaribia kukamilika
- Kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya na Miji, kukamilisha kazi ya upimaji wa mipaka ya vijiji vipya na kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi. Vile vile kuwahamasisha wananchi kuchangia upimaji wa mashamba yao na kuwapatia hatimiliki za kimila, pamoja na kujenga masjala za ardhi katika ngazi za Wilaya na Vijiji.
- Kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi wenye program 12 ambazo ni programu ya kuimarisha TUME, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Misitu, Wanyamapori, Madini, Nishati, Miundombinu, Rasilimali maji, Utalii na Uwanda/Uoto Asili kwa lengo la kukamilisha kazi ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi nchini.
- Kushirikisha Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) katika kufanya tafiti mbali mbali za vifaa vya ujenzi wa nyumba bora kwa teknolojia rahisi na gharama nafuu na kufikisha matokeo ya utafiti huo kwa wananchi.
- Kuhakikisha kuwa jumla ya nyumba 15,000 (kwa wastani nyumba 3,000 kila mwaka) zinajengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kushirikiana na sekta binafsi.
- Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa masharti nafuu, kuwahamasisha wananchi kuzielewa Sheria ili wazitumie kupata mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba na kuhamasisha mabenki na vyombo vingine vya fedha kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba ya muda mrefu na yenye riba nafuu.
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa programu ya Taifa ya Kurasimisha Makaazi nchini. Programu hii itakuwa dira ya kuboresha makaazi na kukabiliana na tatizo la ujenzi holela nchini. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine itaendeleza kasi ya Urasimishaji wa ardhi na nyumba katika Majiji na Hamashauri za Miji na Wilaya na kutoa leseni za makazi.
- Kutekeleza mradi kabambe wa kuweka kituo cha kupokea picha za Satellite (Satellite Imagery Receiving Station) kitakachorahisisha upimaji wa ardhi yote nchini na pia kitarahisisha utayarishaji wa ramani kwa ajili ya matumizi mbalimbali.



