Mifugo na Uvuvi
Serikali ya Awamu ya nne imeendeleza kwa msisitizo zaidi lengo la kuzingatia zaidi ubora kuliko wingi pekee katika ufugaji. Na imelenga kuendeleza sekta ya uvuvi ili ichangie zaidi ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuwaongezea kipato wavuvi.

Katika kipindi kipitacho cha 2005-2010, serikali ya awamu ya nne imezidisha mkazo katika kuzitumia maliasili zilizomo katika bahari, maziwa na mito pamoja na kuendeleza ili wavuvi na wafgaji waweze  kutumia fursa zake na kuinua hali zao za maisha.

1. Uzalishaji wa Maziwa, Nyama na Mayai:

  • Serikali ya awamu ya nne imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa maziwa pamoja na ulaji wake, Usindikaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita 56,580 kwa siku mwaka 2004/2005 hadi lita 88,940 mwaka 2008/09
  • Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita bilioni 1.4 mwaka 2004/06 hadi lita bilioni 1.6 mwaka 2008/09.
  • Uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 378,509 hadi tani 422,230. Uzalishaji wa mayai uliongezeka kutoka mayai bilioni 1.8 hadi mayai bilioni 2.8 mwaka 2008/09.

2. Kuimarisha Uhimilishaji:

  • Tumeanzisha vituo vya uhimilishaji vya  Kanda Mbeya, Mwanza, Kibaha na Dodoma.
  • Tumenunua mitambo minne ya kutengeneza hewa baridi ya Naitrojeni, kwa ajili ya Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) Arusha na vya Kanda.
  • Wizara imenunua madume 10 bora ya mbegu kutoka Afrika ya Kusini yapo kituo cha NAIC Arusha, ambapo wanazalisha dozi 252,985 za mbegu za ng’ombe (semen) na ng’ombe 221,183 wamehimilishwa.
  • Uwezo wa kuzalisha mbegu bora umeongezeka kutoka dozi 50,000 hadi dozi 340,000 kwa mwaka.

3. Uendelezaji wa mashamba, kuimarisha Miundombinu na Masoko ya Mifugo:

  • Serikali imeiwezesha NARCO kuanza ujenzi wa machinjio itakayogharimu shilingi bilioni 10.7 katika ranchi ya Ruvu mkoa wa Pwani. Itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 800 na mbuzi/kondoo 400 kwa siku.
  • Serikali imenunua ng’ombe wazazi 570 na madume 10 kwa ajili ya mashamba ya kuzalisha mitamba
  • Serikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi imesambaza mitamba 24,549 na mbuzi wa maziwa 5,379 kupitia Kopa Ng’ombe/Mbuzi, Lipa Ng’ombe/Mbuzi mikoa yote, mwaka 2004/05 hadi 2008/09.
  • Jumla ya ng’ombe 2,496,829, mbuzi 2,014,353.na kondoo 362,154 wa TAS bilioni 703.9 waliuzwa minadani. Aidha, ng’ombe 13,042 na mbuzi 13,714 wa TAS bilioni 7.9 waliuzwa nje ya nchi. Tani 674.0 za nyama ya ngombe, mbuzi na kondoo za TAS bilioni 2.1 zimeuzwa nje ya nchi.

4. Kuendeleza na kufufua sekta ya ngozi:

  • Mkakati wa Kufufua na Kuendeleza Sekta na Viwanda vya Ngozi umeandaliwa na kutekelezwa katika Halmashauri 55 za mikoa 13 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Mifugo (LDF)
  • Jumla ya vipande vya ngozi milioni 7.12 za ng’ombe, milioni 7.5 za mbuzi na milioni 4.42 za kondoo vilizalishwa na kuuzwa nje ya nchi na kuliingizia Taifa shilingi bilioni 58.0

5. Uendelezaji nyanda za malisho na ufugaji wa asili:

  • Jumla ya malambo 537 na mabwawa 2 yamejengwa ama kukarabatiwa
  • Visima virefu 39 vimechimbwa, sehemu mbali mbali nchini
  • Serikali imewapatia wakufugaji maeneo ya kuchungia wafugaji takriban hekta 1,391,109.41 sawa na asilimia 3.8 hekta milioni 60 za eneo linalofaa kwa ufugaji. Utengaji umefanyika katika vijiji 240 vya Halmashauri za Wilaya 31 za mikoa 13.
  • Uboreshaji wa malisho katika mashamba ya uzalishaji mbegu bora yamezalisha tani 84.4 za mbegu aina mbalimbali na marobota 929,680 ya hei yamesambaza kwa wafugaji. Wazalishaji binafasi wameongezeka kutoka 6 mwaka 2006 hadi 40 mwaka 2008 na wamezalisha tani 18.5 za mbegu bora na marobota 509,980 ya hei.

6. Uthibiti wa magonjwa ya mifugo:

  • Serikali ya awamu ya nne imefanikiwa kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mifugo kama Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Ugonjwa wa Miguu na Midomo, Mafua Makali ya Ndege (HPAI-H5N1)
  • Serikali pia imedhibiti magonjwa ya kuambukiza binadamu kama,Ugonjwa wa Bonde la Ufa, Kichaa cha mbwa, Kutupa mimba (Brucellosis) na Kifua Kikuu cha ngombe (Bovine Tuberculosis)
  • Kiasi cha shilingi bilioni 12.5 zilitolewa kama ruzuku kwa  ununuzi wa dawa za kuogesha mifugo kwenye mikoa yote Tanzania Bara.
  • Tafiti mbalimbali zimefanyika katika sekta ya Mifugo na Uvuvi  Mfano chanjo dhidi ya ugonjwa wa mdondo imeongezeka kutoka dozi milioni 6.8  mwaka 2006 na kufikia dozi milioni 33 mwaka 2009 na kufanya dozi zilizozalishwa kuwa milioni 65.7 za chanjo hiyo, pia dozi 1,765,500 za Kimeta na dozi 336,400 za Chambavu zimezalishwa na kusambazwa. Tathmini imeonyesha kupungua kwa vifo vya kuku wa asili kutoka asilimia 90 hadi asilimia 4 pale ambapo chanjo ya mdondo imetumika.

7. Huduma za Ugani na Mafunzo:

  • Serikali imeongeza idadi ya wanafunzi waliosajiliwa katika vyuo vya Mifugo kutoka wataalam 320 mwaka 2005/2006 hadi 1,222 mwaka 2009/2010 . Hali hii imepunguza pengo la mahitaji ya wataalam wa Mifugo kutoka 13,469 hadi kubakia 11,874.
  • Vyuo vya Uvuvi vimeongeza uwezo wa kudahili wanafinzi kutoka 110 mwaka 2006 hadi kufikia 300 mwaka 2009 ambapo jukla ya wanafunzi hao 553 wamehitimu katika kipindi hicho.

8. Uthibiti wa Uvuvi Haramu,biashara ya magendo na kuongeza mapato ya serikal kutoka sekta ya Uvuvi:

  • Serikali imefanikiwa kudhibiti uvuvi haramu na biashara za magendo ya mazao ya uvuvi katika maziwa, mito na bahari.
  • Pia Serikali imeanzisha  Mamlaka ya Uvuvi katika Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority).
  • Serikali ilifanikiwa kukamata  meli moja kubwa ya uvuvi (TAWARIQ 1) ikivua katika ukanda wa pwani ya Tanzania ni mafanikio katika kudhibiti uvuvi haramu. Wananchi 654  wanaoishi ndani ya maeneo ya hifadhi wamepatiwa mashine za kupachika 12, masanduku 4 ya barafu (ice boxes) kwa ajili ya kuhifadhia samaki, nyavu za jarife vipande 1,214 pamoja na maboti 10. ili kupunguza kasi ya uharibifu wa rasilimali za bahari.

9. Ubora na Usalama wa samaki na mazao ya Uvuvi:

  • Serikali imejenga Maabara ya Taifa ya Nyegezi ya Udhibiti wa Ubora wa Mazao      ya Uvuvi. Maabara hiyo imepata ithibati Na. T 0327 iliyotolewa na South African National Accreditation Services (SANAS) na hivyo kutambulika Kimataifa. Kutokana na kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa, samaki aina ya kamba wanaofugwa katika Wilaya ya Mafia wamepata soko la nje katika nchi za Jumuiya ya Ulaya.

10. Ukuzaji wa Viumbe kwenye Maji na uendelezaji wa Zao la Mwani:

  • Ukuzaji wa viumbe kwenye maji umeongeza na upatikanaji wa samaki na mazao mengine ya majini ambapo vituo 8  vimeboreshwa. Aidha, Uboreshaji wa teknolojia ya ufugaji wa samaki aina ya kambale na kusambaza vifaranga 9,832 vya aina hiyo  kwenye mabwawa ya kuchimba, pia vifaranga  1,799,380 aina ya perege vilisambazwa, kati ya hivyo 624,571 vimepandikizwa kwenye malambo ya asili. Ufugaji wa Kambamiti kibashara umezalisha tani 374.5 zenye thamani ya takribani Dola za Kimarekani 2,351,880. Samaki aina ya  Mwatiko Kilo 370 zenye thamani ya shilingi 1,295,000 zimezalishwa.  Unenepeshaji wa Kaa  unafanyika. kaa wenye thamani ya shilingi 25,000,000 zimevunwa Wilaya ya Pangani. Aidha, Kilimo cha Mwani katika maeneo ya ukanda wa pwani kimeendelea na tani 1172.9 kuzalishwa katika kipindi hicho.

11. Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani:

  • Serikali ya Awamu ya nne imewezesha wananchi wa mwambao wa pwani kushiriki kikamilifu kwenye ulinzi na usimamizi wa malikale, yakiwemo maeneo ya historia kama vile magofu, hii ni katika kuinua kipato cha wananchi pia kuvutia watalii.
  • Hifadhi mpya ya Bahari inayojulikana kama “the Coelacanth Marine Protected Area” iliyopo Mkoa wa Tanga imeanzishwa. Hifadhi hii ni maalum kwa kuonekana kwa wingi kwa “Coelacanth” au kwa Kiswahili ‘’Silikanti’. Eneo hili, ni kivutio kikubwa kwa watalii, wanasayansi na wana harakati wa hifadhi duniani kote.

Comments are closed.