1. SEKTA YA WANYAMAPORI
1.1. Uwindaji wa kitalii umeongeza mapato
- Sekta ndogo ya Wanyamapori iliendelea na utaratibu wa kuzipatia Halmashauri za Wilaya asilimia 25 ya fedha zitokanazo na Uwindaji wa Kitalii uliofanyika katika Halmashauri husika.
- Jumla ya Shilingi 1,822,671,306 zilitolewa katika Halmashauri 44 zenye vitalu vya uwindaji. Aidha, Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (TWPF) ulichangia jumla ya Shilingi 759,673,394 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
1.2. Wananchi wanashiriki katika shughuli za kuhifadhi wanyamapori
- Wizara iliwezesha pia kuidhinisha kwa jumla ya maeneo 10 kuwa Jumuiya kamili za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs). Maeneo hayo ni Burunge (Babati), Ipole (Sikonge), Uyumbu (Urambo), Ngarambe-Tapika (Rufiji), Pawaga-Idodi (Iringa), Ikona (Serengeti), Enduimet (Longido), Nalika (Tunduru), Mbarang’andu (Songea) na Wami-Mbiki (katika wilaya za Morogoro, Mvomero na Bagamoyo).
1.3. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imechangia maendeleo ya wananchi
- Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliendelea kutoa kipaumbele katika kushirikisha wananchi wanaozunguka na waliopo ndani ya eneo la hifadhi katika kusimamia na kunufaika na raslimali za wanyamapori, ambapo miradi mbalimbali ambayo inasimamiwa na Baraza la Wafugaji (Pastoral Council) ilianzishwa.
- Kati ya 2005 na 2009 jumla ya Shs. 3,953,336,140 zilitolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
1.4. Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limechangia katika kuwalete wananchi maendeleo
- Kupitia mradi wa Ujirani Mwema TANAPA imechangia jumla ya Shs 3,070,328,725 kuvileta maendeleo vijiji ambavyo vinapakana na Hifadhi za Taifa.
1.5. Wizara imeongeza juhudi za kulinda Mapori ya Akiba (Game Reserves)
- Jumla ya siku za doria 495,565 zilifanyika ndani na nje ya mapori ya akiba ambapo watuhumiwa 5,285 walikamatwa kwa kuvunja Sheria ya uhifadhi wa Wanyamapori na pia wanyama waharibifu 116 waliuawa katika wilaya mbalimbali.
- Katika kurahisisha usimamizi wa Mapori ya Akiba, jumla ya kilomita 350 za barabara mpya zilitengenezwa ndani ya mapori ya akiba. Wizara ilikarabati pia jumla ya kilomita 982 za barabara pamoja na viwanja 10 vya ndege ndani ya mapori ya akiba.
- Ili kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika mapori ya akiba, Wizara ilijenga jumla ya nyumba kumi za watumishi na ofisi moja katika Pori la Akiba la Rungwa na moja katika Pori la Akiba la Swagaswaga.
- Katika kuwezesha kuwepo kwa uhifadhi na matumizi endelevu ya raslimali za Wanyamapori, Wizara iliandaa mpango wa usimamizi katika mapori ya Akiba ya Selous.
1.6. Uwindaji wa kitalii
- Jumla ya Kampuni 47 zilipewa leseni za uwindaji wa kitalii.
- Pia jumla ya Dola za kimarekani 70,410,004.00 zilikusanywa kutokana na Uwindaji wa Kitalii.
2. SEKTA YA MISITU NA NYUKI
2.1. Usimamizi Shirikishi wa Misitu umefanikliwa
- Katika kuhakikisha jamii zinashirikishwa katika kuhifadhi na kusimamia rasilimali za misitu, jumla ya Wilaya 63 ziliwezeshwa kutekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (Participatory Forest Management) kwenye vijiji 2,328 vyenye jumla ya hekta 4,122,500.
- Aidha, kati ya vijiji hivyo, vijiji 1,457 vinasimamia misitu ya jamii (Community Based Forest Management) yenye jumla ya hekta 2,345,500. Pia vijiji 871 vinasimamia kwa pamoja (Joint Forest Management) misitu yenye jumla ya hekta 1, 777,000.
2.2. Ufugaji nyuki wa kisasa umeendelezwa
- Wizara inatekeleza mpango wa uendelezaji na uboreshaji wa shughuli za ufugaji nyuki katika wilaya 30, kwa lengo la kuwasaidia wafugaji nyuki waweze kufuga nyuki kitaalam ili kupata mazao mengi na yenye ubora unaokubalika katika soko.
- Aidha, mafunzo ya mbinu bora za ufugaji nyuki yalitolewa katika Wilaya za Kibondo, Rufiji, Uyui, Manyoni, Kondoa, na Handeni na kushirikisha wadau wapatao 708. Kutokana na mafunzo hayo, idadi ya wafugaji nyuki imeweza kuongezeka kutoka 1,791 mwaka 2005 hadi 2,500 mwaka 2009. Kati ya hao wanawake ni 762 na wanaume ni 1,738.
2.3. Mauzo ya mazao ya nyuki nje yameongezeka
- Jumla ya tani 2458.696 za nta yenye thamani ya Dola za Marekani $ 9,839,816 ziliuzwa nje. Wakati huohuo jumla ya tani 3,224 za asali yenye thamani ya Dola za Marekani $ 3,999,129 iliuzwa nje.
2.4. Taratibu za kuvuna mazao ya misitu zimeboreshwa
- Ili kupunguza changamoto zinazohusiana na uvunaji wa misitu, mwaka 2007 Wizara iliandaa Mwongozo wa Uvunaji Endelevu na Biashara ya Mazao ya Misitu. Mwongozo huo umezipatia Serikali za Mitaa nguvu zaidi za kusimamia uvunaji endelevu wa raslimali za misitu. Katika kutekeleza mwongozo huo, jumla ya Wilaya 90 ziliwezeshwa kuunda Kamati za Uvunaji za Wilaya chini ya uenyekiti wa Wakuu wa Wilaya.
2.5. Usafirishaji wa mazao ya misitu umedhibitiwa
- Wizara imeanzisha vikosi vya doria katika kanda 8 ili kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu. Jumla ya doria shirikishi 47,000 zilifanywa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kukamata jumla ya magunia 13,626 ya mkaa, mbao 105,500, magogo 650 na nguzo za mikoko 20,268.
2.6. Mafunzo ya misitu yametolewa
- Jumla ya wananfunzi 1044 wamehitimu mafunzo ya fani ya Misitu kutoka Chuo cha Misitu Olmotonyi Arusha na Chuo cha Viwanda vya Misitu Moshi
2.7. Upandaji miti umeongezeka
- Upandaji miti unaofanywa na wananchi umeongezeka ktoka miche 141,170,552 iliyopandwa mwaka 2005 hadi miche 148,187,000 iliyopandwa mwaka 2009.
- Sekta binafsi ya ndani na nje ya nchi imewekeza katika kuanzisha mashamba ya miti. Kampuni ya Green Resource imepanda hekta 4,500 za miti katika Wilaya za Mufindi, Lindi, na Pangani. Wakati huohuo kampuni ya TanWatt katika Wilaya ya Njombe imepanda miti hekta 14,130.6.
3. SEKTA YA UTALII
3.1. Mchango wa Utalii katika pato la taifa umeongezeka
- Utalii ni Sekta inayokua kwa kasi na mchango wake kwenye pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kila mwaka na kwa sasa ni zaidi ya asilimia 17.5. Aidha, sekta huchangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.
- Kutangaza utalii wa Tanzania katika vituo vya Televisheni vya WABC – TV, CNN – America, ‘CNN headline News’ na tovuti ya CNN.
- Ili kukuza mchango wa Sekta ya Utalii katika pato la Taifa, Wizara iliendelea kupanua wigo wa Mazao ya Utalii kwa kuanisha aina nyingine za utalii kama vile utalii wa mikutano, fukwe za bahari, ikolojia na malikale. Baadhi ya mikutano iliyofanyika ni kama ule wa Sullivan na “African Travel Association-ATA.
3.2. Chuo kipya cha utalii kimejengwa
- Wizara imepanua wigo wa masomo katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kuongeza kozi za Stashahada (diploma) kwenye masomo ya hoteli na utalii. Vilevile, Wizara imefungua tawi la chuo hiki mkoani Arusha na kuongeza udahili wa wanafunzi kufikia 270 kwa mwaka.
- Wakatri huohuo, ili kupata wataalam wa kufanikisha maendeleo ya sekta ya utalii hapa nchini, Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa inaendelea na ujenzi wa kampasi mpya ya Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam. Chuo hicho mabacho kitakamilika mwaka 2010 kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 500 kwa mwaka ambao watapatiwa mafunzo ya hoteli na utalii katika ngazi za stashahada na Stashahada.
3.3. Hoteli za kitalii zimepangwa katika madaraja
- Zoezi la kupanga hoteli katika daraja limefanyika katika Mikoa ya Dar-es-Salaam na Pwani. Katika zoezi hili hoteli 203 zilihusishwa ambapo hoteli 99 zilitathminiwa kwa ajili ya kuwekwa katika daraja. Kati ya zilizotathminiwa hoteli 65 zilikidhi vigezo vya kuwekwa katika daraja stahiki na kupewa nyota.
3.4. Uwekezaji katika utalii umepewa umuhimu
- Katika kipindi cha mwaka 2008, maeneo ya fukwe kwa ajili ya uwekezaji yalibainishwa katika Mikoa ya Tanga (Wilaya za Pangani, Tanga, Mkinga na Muheza) na Lindi (Wilaya za Lindi Mjini, Lindi Vijijini na Kilwa).
- Uwekezaji katika huduma za hoteli za Kitalii uliongezeka, hususan katika Mikoa ya Arusha, Manyara, Pwani na Dar es Salaam ambapo idadi ya hoteli imeongezeka kutoka hoteli 237 zenye vyumba 8,004 mwaka 2006 hadi kufikia hoteli 339 zenye vyumba 10,790 mwaka 2008.
4. SEKTA YA MALIKALE
4.1. Sehemu za malikale zimeboreshwa
- Kwa upande wa vituo vya Olduvai Gorge na Laetoli, Wizara imejenga barabara kutokea katika eneo la Esere hadi kituo cha Nyayo za Laetoli pamoja na kujenga makumbusho ya muda na nyumba ya mtumishi.
- Wananchi katika wilaya 14 za mikoa 6 wameshiriki katika mchakato wa ukamilishaji wa kuandaa kabrasha la njia kuu ya kati ya biashara ya utumwa na vipusa ambalo liliwasilishwa rasmi UNESCO mwezi Januari 2009 kama ombi kwa njia hiyo kuorodheshwa katika orodha ya urithi wa dunia.
- Wizara iliandaa pia mipango ya usimamizi wa vituo saba vya njia hii katika maeneo ya Ujiji-Kigoma, Ulyankulu-Tabora, Kwihara-Tabora, Kilimatinde-Singida, Mpwapwa-Dodoma, Mamboya-Morogoro na Bagamoyo-Pwani.
4.2. Maadhimisho ya kimataifa kuhusu malikale yamefanyika Tanzania
- Wizara iliadhimisha Kumbukumbu ya miaka 50 ya uvumbuzi wa fuvu la “Zinjanthropus” ambayo ilihusisha Kongamano la Kimataifa la siku 3 kuanzia tarehe 13 -15/08/2009 na kufuatiwa na uzinduzi wa eneo lilipogunduliwa fuvu la Zinj tarehe 17/08/2009.
- Aidha, Mwezi Oktoba 2009, Wizara iliandaa Kongamano la Kimataifa la Mtawanyiko wa watu wenye asili ya Afrika waliotawanyika duniani. Kongamano hilo lilifanyika Dar es Salaam na Zanzibar tarehe 25 hadi 30 Oktoba 2009.



