Afya
Mafanikio mengi yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa Sera mpya ya Afya iliyopitishwa mwaka 2007; na kuendeleza Mipango Kabambe ya Afya ya Halmashauri, hadi kufikia 2009/10, jumla ya Halmashauri 132 zinatekeleza mipango hiyo.

1. Kuongezeka kwa jitihada za kupambana na magonjwa ya mlipuko;Elimu juu ya magonjwa ya kuambukkiza na yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya kujikinga na magonjwa mapya yanayojitokeza  kama vilel ebola, marbug, Homa ya bonde la ufa na Homa ya mafua makali ya nguruwe.

Wizara imeendelea kuhamasisha jamii juu ya magonjwa milipuko kwa kutoa vipeperushi zaidi ya laki moja kwa nchi nzima pia imetoa  elimu kwa umma kupiti vyombo mbalimbali vya habari kama vile radio, televion, magazeti na mabango ambayo yamebandikwa barabarani yakieleza  mbinu za Kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

2. Kupungua kwa vifo  vya watoto wachanga na Mama wajawazito;

  • Chanjo zimeendelea kutolewa kwa watoto wote bila malipo. Chajo mpya imeongezwa  aina ya ‘HiB Vaccine’  chanjo hii ianajumushwa na chanjo nyingine  4 zilizokuwa zinatolewa kwa pamoja  sasa zimekuwa tano na kuitwa chanjo ya Pentavalent (DPT –HB-Hib). Katika mwaka 2009  watoto waliopata chanjo  ya surua ni asilimia  93%, DPT-HB3  asilimia 85%, OPV asilimia 88%.
  • Huduma za kliniki zimeboreshwa kwa ununuzi wa vifaa vya kupima mimba, uzito, upatikanaji wa dawa, kufundisha watoa huduma
  • Huduma kwa wajawazito na huduma za kujifungua  pamoja na huduma kwa  watoto  chini ya umri wa miaka  mitano  zimeendelea kutolewa  bila malipo aktika vituo vya Serikali.
  • Vifaa mbalimbali vya huduma ya uzazi na kliniki   wakati wa ujazito vimepelekwa katika hospitali 86 na vituo vya afya 50 kwenye mikoa 20.  Aidha machakato wa kupeleka vifaa vya uzazi na kuhudumia watoto  katika vituo 200 vya vya afya unaendelea.
  • Ununuzi wa pikipiki  za miguu mitatu (ambulance) kwa ajili ya usafiri wa kina mama wajawazito unaendelea na pikipiki 400 zitanunuliwa.
  • Ujenzi wa Zahanati  katika  kila kijiji unaendelea kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya  ya Msingi (MMAM).  Kati ya mwaka 2008/09 hadi 2009/10 zahanati 400 na vituo vya afya 78 vimejengwa.

3. Kuimarika kwa vita dhidi ya UKIMWI na Malaria;

  • Hali ya maambukiza nchini kiwango cha asilimia 5.7.% ya watu wenye umri wa miaka 15 – 49 (THMIS 2007 – 2008). Hali hii ni pungufu ukilinganisha kiwango na kiwango cha 7.7.% cha watu wenye umri  kama huo  iliyotolewa  (THIS 2003 – 2004). Hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Kampeni ya upimaji iliyozunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Dr. J. K. Kikwete Julai 2007.
  • Hadi 2009 Disemba Kliniki 909 zinatoa Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI.  Watu waishio na virusi vya UKIMWI 632,086 wamesajiliwa katika kiliniki hizo na 322,783 katik ya hao wanapata dawa za kupunguza makali ya viruasi vya  UKIMWI.
  • Huduma za kupunguza maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto inatolewa katika vituo vya Tiba  3,626
  • Jamii inaendelea kuelimishwa kupitia vyombo mbali mbali vya upatikanaji habari ikiwa ni pamoja na machapisho, sinema vipindi vya radio, Televisheni na sanaa.

Ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu

  • Mwaka 2008 ni takribani 50% ya kaya hapa nchini zilikuwa na vyandarua vyeneye dawa ya  kudumu (NGAO).  Ili kuongeza kasi Serikali imeamua kugawa bila malipo ili ifikapo mwishoni mwaka mwaka 2011  killa sehemu ya kulaala  iwe chandarua chenye dawa ya kudumu.  Mwaka 2008 Serikali ilianzisha kampeni  ya kugawa bila malipo vyandarua  kwa watoto wenye umri  chini  ya miaka 5.  Hadi kufikia mwezi Aprili (2010)   watoto takriban milioni 9 wamegawiwa vyandaru vyenye dawa ya kudumu.  Kampeni hii imekamilika katika mikoa yote.
  • Kuanzia mwezi  wa nane mwaka huu 2010  kuna kampeni ya pili ya kugawa  bila malipo vyandarua  14.6 milioni  kila kaya itapewa vyandarua  viwili  au zaidi,

Upuliziaji wa Viuatilifu Ukoko katika  Kuta

  • (indoor Residual Spraying)
  • Kampeni hii imeanzia mkoa wa Kagera mwaka 2007 katika Wilaya ya Muleba, na Wilaya ya Karagwe 2008.  Mwaka 2009, afua hii ilitekelzwa katika wilaya zote za mkoa wa Kagera kuanzia mwaka huu (mwezi Agosti, 2010 kampeni itaendelea itajumuisha pia mikoa ya Mara na Mwanza.
  • Kampeni hii imeanzia mikoa  ya Kanda ya Ziwa  kwa kuwa  mikoa hii ndiyo inaongoza kwa maambukizi ya malaria ifuatatiwa na mikoa ya Kanda ya Pwani

Tiba  ya malaria  kwa  dawa mseto

  • Dawa mseto kama Alu ndiyo dawa   bora za kutibu malaria kwa sababu ufanisi wake wa kuponya uko juu (aslimia 95%)
  • Hapa nchini wagonjwa wa malaria wanaokwenda kutibiwa katika vituo vya huduma ya afya vya Serikali wanatibiwa bila malipo  au huchangia gharama kidogo kama Sera ya uchangiaji ilivyo.

4. Kutolewa kwa huduma   za upasuaji wa moyo nchini;

  • Wagonjwa 168 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo
  • Wataalam wa upasuaji wa moyo wameongezeka, WAUJ ilipelekea jumla ya wataalam 27, nchini india na Israel kusomea upasuaji wa moyo na sasa wote wamerudi nchini wakiendelea na kutuoa huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
  • Ujenzi wa kituo maalum cha matibabu ya moyo umeanza kaktika hospiotali ya Taifa Muhimbili, WAUJ inashirikiana na Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mrisho J. Kikwete, na unatarajiwa kumalizika miezi kumi na nne ijayo. Kitakuwa ni kituo bora  katika Afrika Mashariki na kati.

5. Kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na upatikanaji wa vifaa vya kisasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini

  • Karibu majengo yote ya Hospitali ya Taifa Muhimbili yamekarabatiwa na vifaa vya kisasa vimekwea vifaa hivyo ni CT Scan ya Kisasa, Magenet Resonance Imaging (MRI) ya kisasa, Digital, radiograph Sysytem, USS na Fluroscopy.  Mashine za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo zimeshafungwa.
  • Vifaa vya kisasa vimewekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
  • Idara ya Huduma za magonjwa  ya Dharura imeimarishwa kwa kuwa na wataalam na vifaa tiba vya kisasa
  • Vituo vingi vya kutolea huduma za afya hapa nchini  vimepatiwa vifaa vya kutibu wagonjwa

6. Kuimarishsa upatikanaji wa haki za watoto

  • Kukarabati majengo na kutoa vifaa katika mahabusi za watoto na shule ya maadilisho Irambo.
  • Kukamilisha ujenzi wa mahabusu ya watoto Mtwara.
  • Kukarabati chuo cha Walezi wa Watoto Kisangara.
  • Kutoa mafunzo kuhusiana na haki za watoto katika jamii.
  • Kuimarisha utaratibu wa utojai huduma kwa watotot walio katika mazingira hatarishi.
  • Kutoa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi
  • Kuweka viwango vya utoaji wa hududma kwa toto walio katika mazingira hatarishi.

7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee

  • Kukamilika kwa sera ya wazee
  • Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
  • Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
  • Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
  • Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
  • Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.



Comments are closed.