Mafanikio
Mafanikio mengi yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa Sera mpya ya Afya iliyopitishwa mwaka 2007; na kuendeleza Mipango Kabambe ya Afya ya Halmashauri, hadi kufikia 2009/10, jumla ya Halmashauri 132 zinatekeleza mipango hiyo.
Serikali kwa kushirikiana na Taasisi, Wakala na Mamlaka za Elimu, Wadau wa Maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali na Wananchi katika ngazi zote imeendelea kujenga shule, Vyuo na Vyuo Vikuu katika maeneo mbalimbali. Ujenzi huu umewezesha kuongezeka kwa nafasi za masomo.
Serikali ya Awamu ya Nne imeendelea kutekeleza azma yake ya kujenga jamii ya watu wenye afya, wanaoheshimu kazi na haki kwa kuzingatia usawa wa jinsia, kwa kutoa mafunzo mbalimbali katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Vyuo Maendeleo ya Jamii nchini kote.
Katika kipindi cha miaka mitano, Serikali iliendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005 ambayo ilibainisha wazi kuwa kilimo cha kisasa ndiyo msingi na sharti muhimu katika kujenga uchumi wa kisasa
serikali kupitia bodi ya utalii imekuwa ikitangaza vivutio vya utalii ndani na nje kwa kutumia mbinu tofauti. kutokana na jitihada hizo idadi ya watalii wanaotembelea vivvutio mbali mbali imeongezeka.
serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha barabara zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani kwa ajili ya ustawi wa uchumi wa nchi yetu na jamii kwa ujumla.
Serikali ya Awamu ya nne imeendeleza kwa msisitizo zaidi lengo la kuzingatia zaidi ubora kuliko wingi pekee katika ufugaji. Na imelenga kuendeleza sekta ya uvuvi ili ichangie zaidi ukuaji wa uchumi wa Taifa na kuwaongezea kipato wavuvi.
kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kipindi kilichopita za kuboresha upatikanaji wa nishati na kukuza sekta ya madini, sekta hizi zimezidi kushamiri na kupata mafanikio ya kunufaisha taifa letu
Tanzania ni moja wa nchi 189 zilizoridhia malengo ya milenia ya mwaka 2000 kama sehemu ya makubaliano ya kimataifa ya pamoja yaliyopitishwa na Mkutano wa Baraza kuu la Umaoja wa Taifa
Mkakati mmojawapo, ambao tayari tunashughulika, ni wa kutambua rasmi rasilimali na biashara za wanyonge ambazo bado ziko kwenye sekta isiyo rasmi ili zitumike kuwafanya wawe washiriki kamili kwenye uchumi rasmi wa taifa"
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2010 – 2015, Chama Cha Mapinduzi kitaitaka Serikali iikuze sekta ya viwanda kutoka asilimia 9.9 ya sasa hadi asilimia 15 mwaka 2015 kwa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo endelevu ya sekta za viwanda, biashara na masoko kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Serikali ya awamu ya nne ni muumini thabiti wa dhana za demokrasia na utawala bora ambazo misingi yake ni madaraka ya wananchi, utawala wa sheria uwabikaji na uadilifu. (vita dhidi ya rushwa)